Bloomberg: Mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya Israel yalisababisha uharibifu mkubwa

Kituo cha habari cha Bloomberg kimekadiria uharibifu uliosababishwa wa nyumba na mali binafsi huko Israel wakati wa shambulio la hivi karibuni la makombora ya Iran kuwa ni karibu dola milioni 40 hadi 53.

Ikizungumzia takwimu za shirika la ushuru la Israel, Bloomberg ilitangaza kuwa katika wiki mbili zilizopita, wamiliki wa nyumba za makazi 2,500 na maeneo ya biashara wamechukua hatua ya kuchukua bima.

Nusu ya ripoti hizi zinahusiana na vitongoji vya kaskazini mwa Tel Aviv.

Kwa mujibu wa Bloomberg, karibu nyumba 1,000 ziliharibiwa katika mji wa Hod Hasharon katikati mwa Israel (Palestina inayokaliwa kkwa mabavu). Shule moja pia imeharibiwa kusini mwa mji wa Tel Aviv.

Kwa mujibu wa Bloomberg, haijulikani ni kiasi gani cha uharibifu ulioripotiwa unahusiana na makombora ya Iran na kiasi gani cha makombora hayo husababishwa na kuanguka kwa makombora ya ulinzi.

Hivi karibuni pia gazeti la Telegraph la Uingereza limeandika kuwa, Iran imethibitisha uwezo wake wa “kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani” na kwamba kinachofuata baadaye huenda “kinaweza kuwa na uharibu mbaya sana.”

Itakumbukwa kuwa awali, utawala wa Kizayuni wa Israel ulijaribu kudogesha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Iran, lakini kwa mujibu wa gazeti la “The Telegraph, “wiki moja baada ya shambulio hilo linalotambuliwa kuwa moja ya mashambulizi makali zaidi ya nchi moja katika historia kwa kutumia makombora ya kisasa ya balestiki, athari kamili ya shambulio hilo “zimedhihirika, haswa baada ya utawala huo kukiri kwamba kambi zake kadhaa za kijeshi zimeshabuliwa.”