Bintou Keita anatoa wito kwa juhudi zote zielekezwe kwa ‘usitishwaji mapigano bila masharti’

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, Bintou Keita ametoa wito siku ya Alhamisi, Machi 27, kuelekeza juhudi zote katika kufikia usitishaji vita bila masharti na kutekeleza Azimio nambari 2773. Alikuwa akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Usalama siku ya Alhamisi wakati wa kikao kifupi kuhusu hali nchini DRC.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

“Ni muhimu kwamba pande zote ziheshimu ahadi yao iliyoelezwa ya kusitisha mapigano na kutafuta suluhu la amani,” Bintou Keita amependekeza.

Alisisitiza utayari wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC kuunga mkono utekelezaji wake, kuunga mkono “angalizi ya usitishaji vita wa kweli” mashariki mwa nchi.

“Ujumbe wa MONUSCO pia uko tayari kutumia uwezo wake kutekeleza usitishaji mapigano unaowezekana,” ameongeza wakati wa mkutano huu.

Mashariki mwa DRC, waasi wa M23, wakiungwa mkono na majeshi ya Rwanda, wanapambana na jeshi la Kongo. Usitishaji mapigano ulijadiliwa na marais wa Kongo na Rwanda wakati wa mkutano wao nchini Qatar wiki iliyopita.

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC pia amesisitiza kuwa MONUSCO inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuwalinda raia katika maeneo yanayodhibitiwa na M23 katika mkoa wa Kivu Kaskazini, hususan kwa kuwapokea maelfu ya watu waliofika kutafuta hifadhi katika mkoa huo katika vituo vyake.

Kukuza mshikamano 

Mkuu wa MONUSCO anasisitiza dhamira ya Tume ya kuunga mkono juhudi za wahusika wote kukuza uwiano wa kijamii na kuzuia kuenea kwa matamshi ya chuki.

Kulingana na Radio OKAPI, Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ametangaza kuwa zaidi ya wapiganaji 2,000 wa kundi la waasi la Zaire huko Ituri wamesalimisha silaha zao kufuatia mashauriano yaliyofanywa tangu mwezi Januari 2025 na Serikali, kwa msaada wa MONUSCO.

“MONUSCO inaendelea kuwalinda raia, kukabiliana na mashambulizi, kutoa makazi ya muda na kusaidia kuwahamisha raia,” amebainisha.

Hata hivyo, alibainisha kuwa “licha ya juhudi kubwa za kikanda na kimataifa, usitishaji vita wa mara moja na bila masharti uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika, Azimio 2773 la Baraza la Usalama na, hivi karibuni, chini ya mwamvuli wa Qatar, bado hautekelezwa.”

“Ni muhimu kwamba pande zote ziheshimu ahadi yao iliyoelezwa ya kusitisha mapigano na kutafuta suluhu la amani,” ameongeza, akitoa shukrani kwa Rais wa Angola na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, Joao Lourenço, “kwa juhudi zake za upatanishi zisizotetereka zinazolenga kurejesha mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda.”

Amehimiza uteuzi wa haraka wa mpatanishi wa Umoja wa Afrika kuongoza jopo la wawezeshaji walioteuliwa na mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC-SADC, kwa nia ya kuratibu na kuunganisha mipango ya upatanishi, kwa kujenga juu ya misingi ya mchakato wa Luanda na Nairobi.

Hali tete ya kiusalama 

Mkuu wa MONUSCO amekariri kuwa hali iliyopo nchini DRC ni ya kutisha, huku muktadha wa kisiasa na kiusalama ukisalia kuwa wa wasiwasi kutokana na  vuguvugu la “Congo River Alliance (AFC) na kundi la Machi 23 (M23), linaloungwa mkono na vikosi vya ulinzi vya Rwanda” kuendelea kudhibiti maeneo mengine mashariki mwa nchi.

AFC/M23 pia imeendelea mpango wake wa kuweka utawala pinzani katika maeneo wanayoshikilia, hivi majuzi ilimteua gavana, makamu wa gavana wawili na meya huko Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini.

Huko Kivu Kaskazini, AFC/M23 imeteua wasimamizi wa fedha na mjumbe wa madini, “ikirejelea uhusiano kati ya migogoro ya silaha na uchimbaji haramu wa maliasili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,” amesema, kulingana na Radio OKAPI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *