Biden aliionya Israel kuepuka maeneo ya nyuklia na mafuta ya Iran
Utawala wa Biden umesema Israel ina haki ya kujilinda na kujibu mashambulizi ya Iran mapema mwezi huu.
Lakini rais aliiambia Israel kuwa hataunga mkono shambulio linalolenga vituo vya nyuklia vya Iran kwa kuhofia kwamba linaweza kusababisha kuongezeka kwa mzozo huo unaozidi kufukuta.
Pia alisisitiza kuwa Marekani haitaunga mkono shambulio la Israel dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Iran.
“Kama ningelikuwa katika hali yao [Israel], ningekuwa nikifikiria kuhusu njia nyingine badala ya kushambulia maeneo ya mafuta ya Iran,” alisema tarehe 4 Oktoba.
Mwezi huu aliitaka Israel kuwa sawia katika kukabiliana na mashambulizi kutoka Iran.
Israel imesema mashambulizi yanayofanyika yanalenga kijeshi nchini Iran.