
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, anayezuru Budapest, amekaribisha uamuzi wa Hungary kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na “kusimama kukabiliana na taasisi hii potovu” siku ya Alhamisi.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
“Umechukua msimamo wa ujasiri na wa kanuni na ninakushukuru, Viktor,” amesema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake na mshirika Viktor Orban.
Hungary yatangaza kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
Hungary imetangaza Alhamisi, Aprili 3, kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), katika siku ya kwanza ya ziara ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu mjini Budapest, ambaye anakabiliwa na waranti ya kukamatwa na mahakama hiyo.
“Hungary inaondoka ICC. “Serikali itaanza mchakato wa kujiondoa, kwa mujibu wa mfumo wa kisheria wa kimataifa,” ametangaza Gergely Gulyas, mkurugenzi wa ofisi ya Waziri Mkuu Viktor Orban, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.