
BEKI wa kati wa matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC Abdallah Kheri ‘Sebo’ ameingia anga za Wasauzi baada ya kuanza kuwindwa na klabu ya Polokwane City ya Afrika Kusini kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho chenye makao jijini Polokwane katika jimbo la Limpopo.
Taarifa za ndani ambazo Mwanaspoti inazo, zinaeleza mmoja wa wawakilishi wa kikosi hicho cha Afrika Kusini anavutiwa na uwezo wa nyota huyo, japo anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa timu nyingine tofauti zinazohitaji pia saini yake.
“Bado sio rasmi ingawa ni kweli kuna wawakilishi wa Polokwane wanaomuhitaji Sebo, japo kama ambavyo ninakwambia na wao wanasema tu nje, ila hawajaleta ofa mezani kwetu ya kuonyesha wanauhitaji na mchezaji kwa sasa,” kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’, alipotafutwa kwa suala hilo, alisema ni habari za mitandaoni, japo suala la kurudishwa tena kikosini itategemea na mahitaji ya benchi lao la ufundi.
“Kwa sasa anacheza Pamba Jiji kwa mkopo, lakini siwezi kusema baada ya mkataba wake huo kuisha tutamrudisha au laah! kwa sababu hayo ni mambo ya kiufundi na itategemea benchi la ufundi lina malengo gani