Beijing yatangaza mazoezi makubwa ya kijeshi katika Mlango-Bahari wa Taiwan

China imetangaza Jumatano kwamba imezindua mazoezi mapya makubwa ya kijeshi katika Mlango-Bahari wa Taiwan, siku moja baada ya luteka ya kijeshi kupiga kizuizi cha kisiwa kinachodaiwa na Beijing.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mazoezi hayo yanalenga “kujaribu uwezo wa wanajeshi katika udhibiti wa eneo, vizuizi vya pamoja na udhibiti, na mashambulizi ya usahihi kwenye malengo muhimu,” Shi Yi, msemaji wa Kamandi ya Mashariki ya jeshi la China, amesema katika taarifa.

Wakati huo  jeshi la China limetangaza Jumatano kwamba limefanya mazoezi”ya kurusha kwa usahihi wa makombora ya masafa marefu” na kufanya “mazoezi kwenye bandari muhimu na miundombinu ya nishati” wakati wa luteka kubwa ya kijeshi kukizunguka kisiwa cha Taiwan.

Vikosi vya kijeshi vya China “vilifanya mazoezi ya kurusha kwa usahihi wa makombora ya masafa marefu” na kufanya “mashambulio ya usahihi kwenye malengo yaliyoigwa kwenye bandari na vituo muhimu vya nishati,” msemaji wa Kamandi ya Mashariki ya jeshi la China Shi Yi amesema katika taarifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *