Beijing inasema ‘dirisha la amani’ lafunguliwa nchini Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amewaambia viongozi wenzake wa G20 kwamba “dirisha la amani” linafunguliwa nchini Ukraine, siku chache baada ya mkutano mjini Riyadh kati ya maafisa wakuu wa Urusi na Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

China imesema kuwa “dirisha la amani linafunguliwa”, kulingana na maoni yaliyoripotiwa siku ya Ijumaa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Wang Yi, katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20 mjini Johannesburg.

“China imeona kwamba wito wa mazungumzo ya amani umeongezeka hivi karibuni, na dirisha la amani linafunguliwa,” amesema siku ya Alhamisi, Februari 20, kulingana na ripoti ya hotuba yake iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China siku chache kabla ya maadhimisho ya mwaka wa tatu wa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, 2022.

Beijing, ambayo haijawahi kulaani Urusi kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine mnamo mwaka 2022, inataka “suluhisho linalofaa na la kudumu ambalo linashughulikia wasiwasi” wa kila upande, wizara ya mambo ya Nje ya China imeainisha.

Ukraine: Zelensky chini ya shinikizo la kukubali kumalizika kwa vita 

Akiwa analengwa na wachunguzi kutoka kwa Donald Trump na Elon Musk, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yuko chini ya shinikizo siku ya Ijumaa kushirikiana “haraka sana” na Marekani ili kukomesha vita na Urusi.

“Rais Trump ni wazi ameshangazwa sana na Rais Zelensky, kutokana na kwamba hakuhudhuria mazungumzo, na hayuko tayari kutumia fursa ambayo tumempa,” amesema Mshauri wa Usalama wa taifa wa Marekani Mike Waltz.

“Nadhani atashiriki mazungumzo baadaye, na natumai haraka sana,” amebainisha.

Maelewano kati ya Moscow na Washington yameibua hofu ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya Marekani na Ukraine, ambayo inategemea sana msaada wa Marekani kupinga uvamizi wa Urusi.

Rais Donald Trump na Rais Volodymyr Zelensky walirushiana vijembe, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa baada ya mazungumzo ya Jumanne kati ya Urusi na Marekani nchini Saudi Arabia, mazungumzo ya kwanza katika ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje katika kipindi cha miaka mitatu.