BDL usipojipanga utapangwa

TIMU tano za Ligi ya Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (BDL), zimeshindwa kuanza mazoezi hadi sasa na kuonekana zitakuwa na wakati mgumu ligi itakapoanza Aprili.

 Timu hizo ambazo ni Dar City, Chui, Savio, DB Oratory, na KIUT hazijaonekana zikijifua kokote kwa maandalizi ya ligi hiyo na hata nyota wake hawakuwepo kwenye mashindano maalumu ya Ramadhan Star Ligi.

Timu 11 ziliingiza wachezaji wake katika mashindano hayo ya Ramadhan na wachezaji waliounda timu nane.

Mastaa hao walitoka timu za UDSM Outsiders, ABC, JKT, Vijana ‘City Bulls’, Kurasini Heat, Pazi, Mchenga Star, Polisi , Stein Warriors, Mgulani JKT na Srelio.

Inaelezwa kushiriki kwa wachezaji wa timu hizo kwenye mashindano hayo, itasaidia kwa timu zao kufanya vizuri katika ligi ya BDL, kuliko zile ambazo hazikuingiza wachezaji.

Wakati huo huo, tarehe ya kuanza kwa ligi hiyo inatarajiwa kutangazwa na uongozi wa BD baada ya kukutana na viongozi wa klabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *