Basata kuja na suluhisho kupunguza migogoro kwa wasanii

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kuwa lipo mbioni kuanzisha muundo wa mikataba ya kazi za muziki, ambao unalenga kupunguza changamoto zinazoikumba sekta hiyo nchini.

Mikataba hiyo ya mfano itakuwa mwongozo kwa wasanii, mameneja wao na kampuni za kurekodi (record labels), kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia ili kusaidia kupunguza matatizo ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika tasnia ya muziki.

Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka BASATA, Abel Ndaga, alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia mikakati ya kutatua changamoto hizo za mikataba ambazo zimekuwa kikwazo kwa wasanii wengi.

“Kumekuwa na changamoto kubwa sana linapokuja suala la mikataba. Sisi kama Baraza la Sanaa tumegundua kuwa mivutano mingi tunayopokea inatokana na mikataba isiyoeleweka vizuri.

 “Kwa hiyo, tunakwenda sasa kama Baraza kuwa na model ya mikataba, ambayo hata kama haitakuwa kamili kwa asilimia mia moja, angalau itasaidia kupitia maeneo muhimu ili kuondoa changamoto ambazo tumeziona.”

Hata hivyo, Ndaga aliwahimiza wasanii kuwa na mazoea ya kufika BASATA kupata ushauri wa kisheria kabla ya kusaini mikataba kwani huduma hiyo hutolewa bila malipo na inasaidia msanii kuelewa masharti ya kisheria ya mkataba anaotarajia kusaini.

“Pindi msanii anaposajiliwa ofisini kwetu, tuna idara ya sheria. Kwa hiyo huwa tunashauri kwamba kabla hajatia saini mkataba wowote, afike Baraza la Sanaa tupitie mkataba huo na kumpa ushauri wa faida na hasara zake,” alisema.

Aidha akizungumza na Mwananchi, msanii wa Hip Hop, Musa Mabumo maarufu kama Bando, alisema kuwa muundo huo wa mikataba ni hatua nzuri ya kuhakikisha usawa katika sekta.

“Nadhani model hizi ziwe za pande mbili zimwangalie msanii na pia mwekezaji anayemuunga mkono. Ziwe na usawa ili isionekane msanii pekee ndiye anayestahili huruma, bali hata mwekezaji apewe haki yake. Hilo litaongeza imani na kuvutia wawekezaji zaidi kwa wasanii,” alisema Bando.

Kwa upande mwingine, meneja wa wasanii, Godfrey Abel, alisema Baraza linapaswa pia kutoa elimu ya ziada kwa mameneja wa wasanii.

“Kuna haja ya BASATA kutoa mafunzo kuhusu wajibu wa meneja katika kumsaidia msanii kukua. Kwa sababu kama meneja hajui wajibu wake, ni rahisi kutosimamia mkataba vizuri, jambo ambalo linaweza kumuumiza msanii,” alieleza.

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza sekta ya biashara ya muziki kwa kuiweka katika mfumo wenye mnyororo mzuri wa maendeleo.

Utakumbuka kauli hii imekuja siku chache baada ya msanii wa Konde Music Worldwide, Ibraah kuomba mchango wa pesa kwa wananchi, aweze kuilipa lebo hiyo ili ajiondoe
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *