Baraza Maalumu: Moshi wa kwanza mweusi katika Vaticani, ambapo makadinali humchagua papa mpya

Makadinali 133 waliopewa jukumu la kumchagua mrithi wa papa Francis wameingia kwenye kongamano siku ya Jumatano, Mei 7, Vatican. Watajadiliana na kupiga kura kumchagua papa wa 267, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani. Duru ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kumpata papa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Kama ilivyotarajiwa, kura ya kwanza ya makadinali waliokusanyika katika Baraza maalumu haikutoa theluthi mbili ya kura, yaani kura 89, zinazohitajika kumteua mrithi wa Francis. Kutoka kwa bomba nyembamba la chuma kilichowekwa kwenye paa Kanisa la Sistine, moshi unaotangaza ambao ulitoka saa 3 usiku saa za Vaticaniu ulikuwa mweusi, ikimaanisha kutokuwepo kwa chaguo. Papa akichaguliwa, moshi utakuwa mweupe. Mzunguko huu wa kwanza juu ya yote umewezesha kupima nguvu zilizopo.

Makadinali hao walikusanyika kwa mara ya kwanza katika sala Jumatano alasiri kwenye Ikulu ya Mitume ya Vaticani. Zaidi ya wiki mbili baada ya kifo cha Jorge Bergoglio, makadinali 133 waliopewa jkumu la kumchagua papa mpya kutoka nchi 70 – idadi ambayo ni rekodi – wamezindua sherehe hii iliyoratibiwa sana, ikifuatiwa kwa makini na baadhi ya Wakatoliki bilioni 1.4 na maelfu ya waandishi wa habari kutoka duniani kote.

Muda mfupi baada ya saa 10 alaasiri saa za Vaticani, walikusanyika kwa ajili ya maombi katika Kanisa la Pauline, mita chache kutoka Kanisa la Sistine Chapel. Huku mikono yao ikiwa juu ya Biblia, waliapa kutofichua chochote kuhusu mazungumzo hayo – chini ya adhabu ya kutengwa na kanisa – kabla ya kujifungia nje mbele ya picha kuu na ya kutisha ya Michelangelo ya Hukumu ya Mwisho. Baada ya kukariri fomula ya ibada pamoja kwa Kilatini chini ya usimamizi wa Kadinali Pietro Parolin wa Italia, “wakuu wa Kanisa” walipishana mmoja baada ya mwingine kuelekea madhabahuni ili kula kiapo, mikono yao ikiwekwa juu ya Injili.

Saa 11:45 jini saa za Vaticani, milango ya Kanisa la Sistine ilifungwa, ikiashiria mwanzo kamili wa mkutano huo. Msimamizi wa sherehe za kiliturujia, Bi. Diego Ravelli, alifunga milango mizito ya kanisa kutoka ndani. Hapo awali, alizindua kwa dhati fomula ya Kilatini “extra omnes” (“wote nje”) ili kuwaondoa nje watu (maafisa, wauguzi, wanadini, n.k.) ambao hawakuidhinishwa kushiriki katika mkutano huu wa faragha.

Kabla ya kuanza kwa ibada hii ya wahenga, makadinali wote walihudhuria misa takatifu asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, iliyoongozwa na Mkuu wa Chuo cha Makardinali, Mtaliano Giovanni Battista Re. Katika mahubiri yake, alitoa wito wa kuchaguliwa kwa papa “ambaye Kanisa na wanadamu wanamhitaji katika kipindi hiki kigumu, cha mabadiliko na mateso katika historia,” na akaomba “kudumishwa kwa umoja wa Kanisa.”

Kwa hivyo uchaguzi huo unatarajiwa kuendelea Alhamisi, huku duru mbili zikipangwa kwa kikao cha asubuhi na mbili alasiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *