Baraza Maalumu la kumchagua Papa kuanza leo Vatican

Makadinali133 wanatarajiwa kuanza kumchagua papa mpya wakati kongamano Makadinali133 wanatarajiwa kuanza kumchagua papa mpya wakati kongamano litakapoanza katika Kanisa la Sistine Chapel Jumatano alasiri na kupiga kura yao ya kwanza.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Makadinali wamehitimisha mikutano yao ya kabla ya mkutano mkuu mjini Vatican, wakijaribu kumtambua papa mpya anayeweza kurithi nafasi ya Papa Francis, aliyefariki Aprili 21 akiwa na umri wa miaka 88.

Makadinali133 watakaopiga kura kutoka nchi 70 wanaonekana kuwa na umoja katika kusisitiza kwamba swali lililo mbele yao sio kubwa kama Kanisa Katoliki litakuwa na kiongozi wake wa kwanza kutoka Asia au Afrika, au kama atakuwa mhafidhina au mwenye maendeleo.

Badala yake, wanasema, kazi kuu ni kupata kiongozi ambaye anaweza kuwa mchungaji na mwalimu, mtu anayeweza kuunganisha Kanisa na kuhubiri amani.

“Tunahitaji mtu mkuu jasiri” amesema Kardinali William Seng Chye Goh, Askofu Mkuu wa Singapore mwenye umri wa miaka 67.

Kazi hiyo ni kubwa, ikizingatiwa unyanyasaji wa kijinsia na kashfa za kifedha ambazo zimeharibu sifa ya Kanisa na mielekeo ya kutokuwa na dini ambayo, katika sehemu nyingi za ulimwengu, inawaondoa watu kutoka kwa dini iliyopangwa.

Kati ya makadinali 133 watakaopiga kura, Papa Francis amewataja 108, lakini hali ya sintofahamu inazingira uchaguzi huo kwa sababu wengi wao hawakujuana kabla ya wiki iliyopita.

Hii ina maana hawajapata muda mwingi wa kuamua ni nani kati yao anayefaa zaidi kuliongoza Kanisa, ambalo lina wafuasi bilioni 1.4.

Makadinali hao walifanya siku yao ya mwisho ya mikutano ya kabla ya mkutano mkuu siku ya Jumanne, ambapo pete na muhuri wa Papa Francis viliharibiwa kama moja ya ibada rasmi za mwisho za mabadiliko kutoka kwa papa hadi mwingine.

Makadinali hao wataanza mchakato wa kumchagua papa mpya wakati kongamano litakapoanza katika Kanisa la Sistine Chapel siku ya Jumatano mchana na makadinali kupiga kura yao ya kwanza.

Waumini na wafuatiliaji wengine kote duniani watasubiri ishara ya kuchaguliwa kwa papa mpya kupitia moshi utakaotoka kwenye chimni iliyofungwa juu ya kanisa la Sistine.

Moshi mweupe utakapofuka itakuwa ni ishara kuwa baraza hilo la makadinali limefanikiwa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *