Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa kesho Jumatatu litaitisha kikao kujadili mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
Amir Saeid Iravani Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la UN na kuyataja mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran kuwa yanakiuka pakubwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya nchi hii. Amesema hujuma za Israel dhidi ya Iran ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Balozi wa utawala wa Kizayuni katika Umoja wa Mataifa ametoa madai haya akijibu ombi la Tehran kuwa, kufanyika kikao cha Baraza la Usalama la UN hapo kesho ni katika juhudi za Iran za kuidhuru Israel.
Katika hatua ya kuibua mivutano na machafuko, utawala wa Kizayuni jana alfajiri ulishambulia baadhi ya kambi za kijeshi katika mikoa ya Tehran, Khuzistan na Ilam ambapo mfumo wa ulinzi wa anga wa Iran ulifanikiwa kuzima hujuma hiyo na kukabiliana na hatua za kichokozi za utawala wa Kizayuni.