Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kupitia Kikundi Kazi cha Kilimo, limekuja na maazimio kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo hapa nchini, sambamba na kuifanya sekta hiyo kuchangia uchumi wa Taifa ipasavyo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa pili uliojumuisha viongozi kutoka idara mbalimbali za Serikali na sekta binafsi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kikundi Kazi hicho ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema lengo la mkutano huo ni kujadili mafanikio yaliyopo katika sekta hiyo na changamoto ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi kwa pamoja kati ya sekta hizo mbili.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates