Mawaziri wa Baraza la Mawaziri la Somalia wiki hii lilimfukuza kazi mkuu wa vikosi vya jeshi Ibrahim Sheikh Muhyadin Addow, na kumteua Meja Jenerali Odowaa Yusuf Rageh kushika wadhifa huo.
Somalia imefanya mabadiliko hayo wakati wa mkutano wa dharura mjini Mogadishu huku kukiwa na mvutano wa kisiasa unaoongezeka katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.
Rageh, ambaye hapo awali alihudumu kama mkuu wa jeshi kuanzia mwaka 2020 hadi 2023, aliongoza operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa al-Qaeda chini ya “vita vya pande zote ” dhidi ya kundi hilo vya Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud.

Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia imeeleza kuwa, kuteuliwa tena Rageh kunalenga kuharakisha hali ya usalama na ulinzi wa Somalia na kufutilia mbali magaidi wa al Shabaab ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi dhidi ya serikali na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika tangu mwaka 2007.