Barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam imeshuhudiwa kuwa na msongamano mkubwa wa magari, hali iliyosababisha usumbufu kwa watu…

Barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam imeshuhudiwa kuwa na msongamano mkubwa wa magari, hali iliyosababisha usumbufu kwa watu…

Barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam imeshuhudiwa kuwa na msongamano mkubwa wa magari, hali iliyosababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

#AzamNews imefika eneo hilo kufuatilia hali hiyo kwa karibu, ambapo baadhi ya madereva na abiria wameeleza adha wanayoipata kila siku kutokana na foleni hiyo, wakiiomba Serikali na mamlaka husika kuchukua hatua madhubuti kutatua tatizo hilo kwa haraka.

Aidha watumiaji wa barabara hiyo wamependekeza kuongezwa kwa njia mbadala, kuboreshwa kwa udhibiti wa trafiki au kuharakishwa kwa miradi ya kupunguza msongamano jijini.

#azamnewsupdates
✍@joempangala
Mhariri| @official_jennifersumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *