Dar es Salaam. Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Kilimanjaro umetangaza kufungwa sehemu ya Barabara Kuu ya Himo Njia Panda – Moshi – KIA Njia Panda kuanzia jana Machi 28, 2025.
Hatua hii imechukuliwa ili kuruhusu matengenezo baada ya uharibifu uliosababishwa na bomba kubwa la maji safi lililopo karibu na mzunguko wa Arusha (Arusha Roundabout).

Sehemu ya Barabara Kuu ya Himo Njia Panda – Moshi – KIA Njia Panda inapofanyiwa matengenezo. Picha na Janeth Joseph
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Ijumaa Machi 28, 2025 na Meneja wa Tanroads Mkoa wa Kilimanjaro, magari makubwa yenye uzito wa zaidi ya tani 10 yanashauriwa kutumia barabara mbadala ya Lucy Lameck – Ghaha – Viwanda – Manyema – Mafuta – Nyerere – Bonite – Khambaita.
Kwa upande wa magari madogo, madereva wanashauriwa kutumia barabara ya YMCA – Kilimanjaro kupitia Bustani Alley.

Sehemu ya Barabara Kuu ya Himo Njia Panda – Moshi – KIA Njia Panda inapofanyiwa matengenezo. Picha na Janeth Joseph
Madereva na watumiaji wa barabara wanaombwa kuwa wavumilivu wakati wa kipindi cha matengenezo na kufuata maelekezo ili kuepuka usumbufu.
Endelea kufuatilia Mwananchi.