Banka aukubali mziki wa Kagoma

KIUNGO wa zamani wa Simba na Yanga, Mohammed Banka amesema anakoshwa na uchezaji wa kiungo mkabaji wa Simba, Yusuf Kagoma anayekaba mtu na mtu jambo ambalo ni gumu kwa wapinzani kupenya eneo analolicheza.

Banka alikuwa anacheza kiungo namba sita kama Kagoma jambo linalomshawishi kumfuatilia zaidi aina ya ukabaji wake na kutuliza presha eneo la kati.

“Aina ya wachezaji kama Kagoma ni wachache kwa nyakati za sasa, ila  kitu ninachoweza kumshauri afanye sana mazoezi yake binafsi yatakayomfanya awe bora na fiti muda wote,” alisema.

“Simaanishi Kagoma asinyumbulike maana hata mimi nilikuwa nafunga kwa kupiga mashuti ya mbali. Kinachonifurahisha zaidi haumpiti kirahisi eneo analokuwepo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *