
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Bangladesh sawa na nchi nyingine nyingi za Kiislamu imelaani kitendo cha kichokozi cha utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Bangladesh imetoa taarifa ikilaani kitendo cha kichokozi cha utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran na kutangaza kuwa, Bangladesh inataka wahusika wa kieneo na kimataifa kuzuia kushadidi mivutano kwa kutumia ushawishi wao.
Katika taarifa hiyo, Bangladesh imesisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria za kimataifa, mazungumzo na kuheshimu mamlaka ya nchi na kutoa wito wa kuweko juhudi za kimataifa kwa ajili ya kuunga mkono utulivu katika eneo la Magharibi mwa Asia.
Uhusiano wa umma wa ulinzi wa anga wa Iran ulitangaza katika taarifa: Siku ya Jumamosi, tarehe 26 Oktoba, katika hali ya wasiwasi, utawala wa Kizayuni ulishambulia vituo vya kijeshi katika mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam.
Idara ya Mahusiano ya Umma ya Ulinzi wa Anga wa Iran ilitoa taarifa ikisema kuwa Jumamosi alfajiri utawala wa Kizayuni wa Israel umeshambulia vituo vya kijeshi vya mikoa ya Tehran, Khuzestan na Ilam ikiwa ni katika kuzidisha hali ya mvutano katika eneo, ambapo mfumo wa ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeweza kukabiliana kwa mafanikio na kitendo hicho cha kichokozi cha utawala wa Kizayuni.