Balozi wa UN aionya US kuiweka Ansarullah kwenye orodha ya magaidi

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, Hans Grundberg ameonya kuhusu athari mbaya za Marekani kuitambua Harakati ya Ansarullah ya Yemen kuwa kundi la kigeni la kigaidi, kutokana na mashambulizi ya kundi hilo la Muqawama ya kulipiza kisasi dhidi ya maeneo ya Israel.