Balozi wa Iran UN: Maghala ya nyuklia ya Israel ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa kikanda na wa ulimwengu mzima.