
Donald Trump ametia saini agizo la kiutendaji siku ya Alhamisi, Aprili 24, lenye lengo la kufungua uchimbaji mkubwa wa madini katika kina kirefu cha bahari, ikiwa ni pamoja na katika maji ya kimataifa, changamoto kwa Mamlaka ya Kimataifa ya Bahari (ISA), ambayo kinadharia ina mamlaka juu ya bahari kuu.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii kali ya Marekani na Rais wake Donald Trump imeibua sintofahamu miongoni mwa makundi ya kulinda mazingira, ambayo yanaonya juu ya uharibifu ambao uchimbaji huo unaweza kusababisha kwa mifumo ya ikolojia ya baharini. Maandishi hayo yanamtaka KatibuWaziri wa Biashara Howard Lutnick “kuharakisha ukaguzi” wa maombi “na utoaji wa vibali vya uchunguzi na uchimbaji” wa madini “mbali na ya mahakama za Marekani.”
Pia yamemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani Doug Burgum kufanya vivyo hivyo kwa maji ya eneo hilo. Mpango huo unatarajiwa kukusanya tani bilioni moja za madini katika kipindi cha miaka kumi, afisa mkuu wa Marekani amesema. ISA ina mamlaka juu ya bahari katika maji ya kimataifa, chini ya mikataba ambayo Marekani, hata hivyo, haijawahi kupitishwa. Agizo hilo pia linaelekeza Waziri wa Biashara kutayarisha ripoti juu ya “uwezekano wa utaratibu wa kugawana” kwa mapato ya baharini.
“Kwa kuanza kuchimba madini katika maji ya kimataifa, kwa kuvunja sheria za kimataifa, serikali inafungua njia kwa nchi nyingine kufanya hivyo,” Jeff Watters, makamu wa rais wa shirika lisilo la kiserikali la Ocean Conservancy, amesema katika taarifa yake. “Na hii itakuwa na matokeo mabaya kwetu sote na kwa bahari ambayo tunaitegemea,” ameonya.
Hakuna uchimbaji wa madini wa kibiashara bado umefanyika katika kina kirefu cha bahari, Marekani au kwingineko. Baadhi ya nchi, hata hivyo, tayari zimetoa vibali vya utafutaji katika maeneo yao ya kipekee ya kiuchumi, hasa Japani na Visiwa vya Cook. Utawala wa Trump unakadiria kuwa uchimbaji wa madini kwenye kina kirefu cha bahari unaweza kutengeneza nafasi za kazi 100,000 na kuongeza dola bilioni 300 kwa pato la taifa la Marekani (GDP) katika kipindi cha miaka 10, afisa mmoja amesema. “Tunataka Marekani iwe mbele ya China katika eneo hili,” chanzo kimesema.
Uchimbaji huo unahusu vinundu vya polimetali, aina ya kokoto inayopatikana chini ya bahari, yenye madini mengi kama vile manganese, nikeli, kobalti, shaba na ardhi adimu. Hizi ni metali zilizo na sifa za sumaku ambazo huthaminiwa sana kwa magari ya umeme, paneli za jua, lakini pia simu mahiri na kompyuta ndogo. Marekani ni nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa ardhi adimu, lakini iko mbali sana na China na kwa sasa ina akiba inayokadiriwa kuwa ndogo sana ikilinganishwa na amana za China, Brazili, Australia au India.
Utajiri unazidi kutamaniwa
“Marekani inakabiliwa na changamoto isiyokuwa ya kawaida ya kiuchumi na usalama wa kitaifa: kupata vifaa vyake muhimu vya madini bila kutegemea wapinzani wa kigeni,” agizo hilo linasema. Mnamo 2023, wanachama 31 wa Congress, wote wa Republican, walituma barua kwa Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin wakidai kwamba utawala wa Biden uruhusu uchimbaji madini chini ya maji. “Hatuwezi kuruhusu China kuchukua na kuchimba rasilimali za bahari,” waliandika. Serikali haikujibu hadharani.
Kampuni ya Kanada The Metals Company (TMC) ilitangaza mwaka wa 2025 nia yake ya kukwepa ISA kwa kutafuta idhni kutoka Marekani ili kuanza uchimbaji wa madini kwenye kina kirefu cha bahari. “Huu ni mfano wa wazi wa makampuni ya madini yanayotanguliza akili ya kawaida,” alisema Katie Matthews wa chama cha Oceana.
Mnamo Julai 2024, Gavana wa Kidemokrasia wa Hawaii, Josh Green, alitia saini kuwa sheria mswada wa kupiga marufuku uchimbaji madini katika eneo la maji la jimbo hilo katikati ya Bahari ya Pasifiki. Mashirika mengi ya mazingira yanapinga uvunaji wa madini, yakishutumu kwa kutishia pakubwa mfumo wa ikolojia wa baharini. “Trump anaweka wazi mojawapo ya mifumo ikolojia dhaifu na isiyojulikana kwa uchimbaji usiodhibitiwa wa kiviwanda,” amesema Emily Jeffers, mwanasheria wa Kituo cha Biolojia Anuwai (CBD), akibainisha kuwa zaidi ya nchi 30 zinaunga mkono kusitishwa kwa mpango huo. “Bahari kuu ni yetu sote,” ameongeza, “na kuilinda ni wajibu kwa wanadamu.”