
Nigeria. Mwanamuziki wa Nigeria, Innocent Idibia ‘2Face’ ametangaza kutengana na aliyekuwa mkewe Annie Idibia baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 13.
Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inamuonesha 2Baba akithibitisha utengano wao.
Kabla ya video hiyo chapisho la kwanza la msanii huyo kwenye mtandao wa Instagram lilisomeka, “Hallo kwa watu wangu wazuri kweli, jambo hili ninalopaswa kusema ni fupi lakini pia refu. Mimi na Annie Macaulay tumetengana kwa muda sasa na kwa sasa tumewasilisha kesi ya talaka.
Ningetoa taarifa kwa vyombo vya habari hivi karibuni ili kusema hadithi yangu. Sio kwa sababu ni haki ya mtu yeyote kujua kuhusu maisha yangu ya kibinafsi lakini kwa sababu ninawapenda watu wangu na ninahitaji wajue kutokuwa na hatia au kosa langu. Endelea kubarikiwa watu wangu. Nawapenda nyote,” liliandikwa kupitia ukurasa wa 2face.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye, iliwekwa taarifa nyingine kwenye akaunti hiyo ikidai kuwa ukurasa huo ulikuwa umedukuliwa kwa hiyo ujumbe huo upuuzwe.
Ilisomeka, “Akaunti yangu ya Instagram imedukuliwa, juhudi zinafanywa kurudisha.Nawapenda!”
Katika hali ya kushangaza, 2face baadaye alitoa video kufafanua hali hiyo na kuweka wazi kuwa akaunti yake haikudukuliwa kama taarifa ya awali ilivyosema na alidokeza kuwa chapisho la awali kuhusu kutengana na aliyekuwa mkewe lilikuwa la kweli na sasa wapo kwenye utaratibu wa kupeana talaka.
Utakumbuka kuwa Annie ni miongoni mwa washiriki wa shoo ya Young Famous and African inayorushwa Netflix akiwa na washiriki wengine kama vile Zari Hassan, Khanyi Mbau, Swanky Jerry, Nadia Nakai, Andile Ncube, Diamond Platnumz
na Naked DJ