
Baada ya kuuteka mji wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mwishoni mwa juma hili, kundi hli lenye silaha linaloungwa mkono na Rwanda linaendelea na mashambulizi yake. Siku ya Jumanne, Februari 18, limechukuwa udhibiti wa mji wa Kamanyola,ulio mapakani na Rwanda, mji ulikuwa ukilindwa vya kutosha na jeshi la Kongo na vikosi vya Burundi.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanaendelea na mashambulizi yao mashariki mwa DRC. Baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mwishoni mwa juma hili, waliingia, siku ya Jumanne, Februari 18, Kamanyola, mji ulioko takriban kilomita hamsini kuelekea kusini ambako jeshi la Kongo na vikosi vya Burundi vikilinda.
Kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani, mapigano ya silaha nzito na nyepesi yaliyochukua zaidi ya saa moja yalizuka majira ya alasiri kati ya wapiganaji wa M23 na wanajeshi wa Burundi. Baada ya hapo, askari wa Burundi walionekana wakitoka katikati ya Kamanyola kuelekea uwanda wa Ruzizi.
Jeshi la Kongo, kwa upande wake, lilikuwa tayari limerudi kusini zaidi, hadi Uvira. Kulingana na vyanzo vya ndani, utulivu ulikuwa umerejea siku ya Jumanne jioni. Kituo cha mpakani na Rwanda na kwenye barabara ya kuelekea Burundi, Kamanyola ni eneo muhimu ambalo 80% ya watu walikimbia siku zilizopita.
Wasiwasi watanda Lubumbashi
Wakati maendeleo haya ya M23 yanawatia wasiwasi Wakongo wote, wakazi wa Lubumbashi, mji wa pili kwa ukubwa nchini DRC ulioko kusini-mashariki mwa nchi hiyo, wana wasiwasi mkubwa na wanaitaka serikali kufanya kila linalowezekana kurejesha uadilifu wa eneo hilo. Katikati ya jiji, hali ya usalama na kibinadamu huko mashariki ndio kiini cha mazungumzo yote, anaripoti mwandishi wetu Joseph Kahongo.
“Nina wasiwasi sana kuhusu adhabu waliyopewa raia wenzetu mashariki mwa DRC,” Aaron Mwamba, dereva wa teksi amesema. Mwanasiasa wa upinzani Serge Mukendi pia ameguswa na habari kutoka uwanja wa vita na kutoa wito kwa serikali kuchukua hatua zinazohitajika. “Kisiasa kuna mambo mengi ya kusema kuhusu hali hiyo, lakini mimi kama mwananchi kwanza nawaonea huruma wananchi wenzetu wanaopoteza maisha kwa njia isiyokubalika. Ni wakati wa viongozi wetu kuwajibika! “anasema, huku akiongeza kwamba wasiwasi unaoongezeka katika jiji hilo unahusishwa na imani kwa jeshi la Kongo. “Hatujui uasi huu utakomea wapi na, zaidi ya yote, hatujui ni nini mipango ya serikali”.