Baada ya kuanguka AU, nini Mustakabali wa Odinga na Siasa za Kenya?

Kuingia kwenye siasa za Afrika kupitia uchaguzi wa AUC, kunaonekana na baadhi kama kutamuongezea nguvu kwenye siasa za Kenya, ingawa kuna mtazamo mwingine kuwa, kushindwa kwake, kunakwenda kupunguza mvuto wake kwenye siasa za kiwango cha bara (Afrika) na hilo linasogea pia mpaka kwenye siasa za ndani za Kenya.