Baada ya HAMAS, Jihadul Islami nayo yaishukuru Iran kwa msaada wake mkubwa kwa Palestina

Msemaji wa Brigedi za Al-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imeishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuishambulia mara mbili Israel katika operesheni za Ahadi ya Kweli Moja na Ahadi ya Kweli Mbili na kusisitiza kuwa, Muqawama utaheshimu usitishaji vita kama adui Mzayuni naye ataheshimu makubaliano hayo.