Aucho akoleza mzuka Yanga

KIKOSI cha Yanga kimesharejea jijini Dar es Salaam kikitokea Pemba, Zanzibar kilipoenda kushiriki michuano ya Kombe la Muungano na kuibuka mabingwa kwa kuifunga JKU kwa bao 1-0, huku kiungo wa timu hiyo, Khalid Aucho akikoleza mzuka.

Kiungo huyo tegemeo raia wa Uganda, aliumia Aprili 7 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union ambapo watetezi hao, waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Pacome Zouzoua na kumfanya akose mechi mbili zilizofuata za ligi dhidi ya Azam FC na Fountain Gate.

Hata hivyo, taarifa njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba Aucho aliyekuwa anasumbuliwa na jeraha la nyama la pja, ameanza mazoezi ikiwa ni ishara ya kuiwahi mapema mechi nne zilizosalia za kumaliza msimu ikiwamo Dabi na huenda kaanza kwanza na Namungo iliyopangwa kupigwa Mei 13.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aucho amethibitisha tayari amepona na amerudi katika hali ya utimamu akianza mazoezi mepesi na anaushukuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *