AU yatakiwa kuchukua hatua dhidi ya Mali kwa madai ya ukiukaji wa haki za watu

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa wito kwa nchi za Umoja wa Afrika, kuchukua hatua za haraka dhidi ya uongozi wa kijeshi nchini Mali, unaoendelea kuwanyanyasa wanasiasa wa upinzani na wanaharakati.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kupitia barua iliyotumwa kwa Tume ya Umoja huo kuhusu haki wa binadamu, Human Rights Watch inasema, imechukua hatua hiyo baada ya watu 11 kukamatwa na kuzuiwa kwa kuukosoa uongozi wa kijeshi.

Tangu jeshi lilipochukua madaraka 2020 na 2021 nchini Mali, uongozi wa kijeshi umeendelea kuwalenga wapinzani, wanahabari, wanaharakati na watu wenye mitazamo tofauti hali ambayo imesababisha mazingira magumu ya kisiasa.

Coronel Assimi Goïta- Kiongozi wa kijeshi wa Mali.
Coronel Assimi Goïta- Kiongozi wa kijeshi wa Mali. AFP – OUSMANE MAKAVELI

Daouda Magassa, ni miongoni mwa wakosoaji wakuu wa uongozi wa kijeshi ambao wamekamatwa baada ya kuukosoa uongozi wa kijeshi na kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa urais.

Jeshi lilikuwa limeahidi kufanyika kwa uchaguzi wa urais mwezi Machi mwaka 2024 lakini hilo likaishirishw kwa muda usiojulikana