AU yakaribisha mazungumzo ya Doha kati ya viongozi wa DR Congo na Rwanda

Umoja wa Afrika (AU) umekaribisha mazungumzo katika mji mkuu wa Qatar, Doha, kati ya wakuu wa nchi za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku mapigano yakiendelea katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa DRC.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Mwenyekiti wa AU Mahamoud Ali Youssouf alizipongeza nchi zote mbili “kwa kujitolea kwao katika mazungumzo” na kuzitaka pande zote “kudumisha juhudi hizo.”

Chombo cha kikanda “kinasalia na uthabiti katika kuunga mkono suluhu zinazoongozwa na Waafrika kwa changamoto za Afrika. … Mijadala ya Doha, iliyofanyika kwa nia ya ushirikishwaji wenye kujenga, inalingana na juhudi hizi na inayosaidia taratibu zinazoendelea za kikanda,” Youssouf amesema.

Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, walikutana mjini Doha siku ya Jumanne kufanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kuteka miji miwili mikubwa mashariki mwa DRC mwaka huu.

Viongozi hao walitoa taarifa iliyotaka “kusitishwa kwa mapigano mara moja na bila masharti,” maelezo ya utekelezaji wake yatafafanuliwa “katika siku zijazo.”

Tangazo

Mazungumzo katika taifa hilo la Ghuba yalifanyika baada ya wawakilishi wa M23 kujiondoa katika mkutano uliopangwa kufanyika na maafisa wa DRC nchini Angola siku ya Jumanne baada ya Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo baadhi ya wanachama wakuu wa kundi hilo akiwemo kiongozi Bertrand Bisimwa. EU pia iliwawekea vikwazo makamanda watatu wa kijeshi wa Rwanda na mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini nchini humo, ukiishumu kuunga mkono M23.

M23 ni mojawapo ya zaidi ya makundi 200 yenye silaha yanayopigania udhibiti wa eneo la mashariki mwa DRC, ambalo lina madini ya thamani kama vile kobalti. Serikali ya Kongo, Marekani na kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, madai ambayo Kigali inakanusha.

Baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya muongo mmoja, kundi hilo lilianza tena mashambulizi yake mashariki mwa DRC mwaka 2022 na kuzidisha mashambulizi yake mwezi Januari, na kuuteka mji wa kimkakati wa Goma, ukifuatiwa na Bukavu mwezi Februari.

Vita mashariki mwa DRC vimesababisha moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani kwa watu milioni 7, wakiwemo watoto wasiopungua milioni 3.5, kulingana na Umojawa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *