AU yahofia vita vipya jimboni Tigray Kaskazini mwa Ethiopia

Umoja wa Afrika, unatiwa mashaka na hali ya wasiwasi inayoshuhudiwa katika jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia inayoweza kuzua vita vipya.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya AU, imesema mgawanyiko uliozuka kati ya viongozi wa Tigray unatishia kuvunjika kwa mkataba wa amani wa mwaka 2022.

Mkataba huo uliosainiwa jijini Pretoria, ulisaidia kumaliza vita vilivyodumu  kati ya mwaka 2020-2022 na kuhusisha wapiganaji wa Tigray na vikosi vya serikali na kusababisha vifo vya watu 600,000.

“Tunaomba kuheshimiwa kwa mkataba huo wa amani, ili kuhakikisha kuwa kuna mazingira mazuri ya kuendelea kuwepo kwa amani na maridhiano,” Umoja wa Afrika umesema.

Wito huu wa Umoja wa Afrika, unakuja baada ya rais wa mpito wa jimbo hilo Getachew Reda, kuonya kuwa, huenda kukatokea kwa vita vipya baada ya kundi lingine la Tigray, lililotangaza kujitenga mwezi Agosti mwaka 2024, kuchukua mji muhimu katika eneo hilo hivi karibuni.

Reda, amelishtumu kundi hilo kwa kuazisha ushirikiano na vikosi vya kigeni hasa Eritrea, hali ambayo huenda inazua  wasiwasi zaidi.

Wakati hayo yakijiri, kuna wasiwasi wa kutokea tena kwa vita vipya kati ya Ethiopia na Eritrea, hali inayotishia hali ya usalama na kibinadamu katika ukanda wa pembe ya Afrika.

Naye Jenerali Tsadkan Gebretensae, makamu wa rais katika jimbo la Tigray katika ujumbe wake ulioandikwa kwenye Jarida la The Africa Report siku ya Jumatatu, ameonya kuwa vita kati ya nchi hizi mbili huenda vikatazuka tena kwa sababu ya mzozo unaoshuhudiwa.

Uhusiano kati ya Ethiopia na Eritrea umeendelea kuwa wa mashaka baada ya nchi hiyo kujitenga mwaka 1993, baada ya vita vya miaka 30.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *