AU: Morocco na Algeria zaonyesha ushindani wao katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi muhimu

Umoja wa Afrika unapokutana Ijumaa, Februari 14 mjini Addis Ababa, ushindani kati ya mataifa ya kupata nafasi ndani ya taasisi za umoja huo unashuhudiwa, hasa kati ya Algeria na Morocco. Majirani hao wamevunja uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 2021 na utambuzi wa Washington wa mamlaka ya Morocco juu ya Sahara Magharibi. Kwani Algiers, inayounga mkono kwa dhati wa vuguvugu la kupigania uhuru wa Polisario, inatafuta kurejesha ushawishi wake uliopotea katika Umoja wa Afrika.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Addis Ababa, Clothilde Hazard

Mnamo Jumatano, Februari 12, duru ya kwanza ya pambano kati ya Rabat na Algiers ilimalizika kwa suluhu. Algeria ilikuwa inatafuta kiti katika Baraza la Amani na Usalama, chombo muhimu cha AU, nafasi ambayo sasa inakaliwa na Morocco kwa miaka mitatu. Ushawishi wa pande zote mbili ulisababisha uchaguzi kuahirishwa, na hakuna upande uliofanikiwa kupata theluthi mbili ya kura, na kuacha wazi kiti kilichotengwa kwa Afrika Kaskazini.

Mchuano huo unaendelea, huku mpambano mpya ukitayarishwa kwa wadhifa wa kimkakati wa makamu wa rais wa Tume, atakaychaguliwa mwishoni mwa juma hili. Wagombea wawili wanaopewa nafasi zaidi ni balozi wa Algeria katika AU, Selma Haddadi, na Mmorocco Latifa Akharbach, rais wa Mamlaka ya Juu ya Mawasiliano na Vyombo vya habari nchini Morocco. Nchi zote mbili zinajishughulisha na kampeni kali yenye matokeo yasiyo na uhakika. “Ni vurugu tupu,” amebaini mmoja wajumbe wa Morocco, “uchaguzi katika Baraza la Amani na Usalama (PSC) umetuonyesha kwamba baadhi ya wapiga kura hawatimizi ahadi zao, kura zao zinaweza kubadilika mara moja.”

Ili kuunga mkono dhahiri zeoezi hili haiba, Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune atakuwepo mwenyewe kwa mkutano huo mwishoni mwa juma hili. changamoto ni kubwa: Makamu wa Rais wa Tume ana majukumu makubwa. Na hii ingezuia Algeria kutengwa katika taasisi hiyo.