Askari wengine 144 wa Kenya wapelekwa Haiti kusaidia kurejesha usalama na utulivu nchini humo

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen, amesema jukumu la kudhamini usalama linalotekelezwa na kikosi cha usaidizi cha mataifa kadhaa (MSS) kikiongozwa na nchi hiyo huko Haiti linazidi kuimarishwa na kupata nguvu zaidi ikiwa ni uthibitisho wa namna taifa hilo la mashariki ya Afrika linavyotimiza ahadi yake kwa Jamii ya Kimataifa.