Askari wa Israel wavamia misikiti mjini Nablus na kuzuia Swala ya Ijumaa

Vikosi vya jeshi la Israel vimevamia misikiti kadhaa katika mji mkongwe wa Nablus, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuzuia kuswaliwa Swala ya Ijumaa.