Askari idara ya misitu matatani tena kwa mauaji 

Dar es Salaam. Baada ya watumishi saba wa idara ya misitu kushikiliwa na Jeshi la Polisi mwaka 2024 kwa tuhuma za mauaji, wengine wawili wanashikiliwa kwa tuhuma hizo kwa tukio linalodaiwa kutokea Februari 28, 2025.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani katika taarifa kwa umma iliyotolewa Machi 6, 2025, linaeleza linawashikilia askari wawili wa idara hiyo iliyo chini ya Wa-kala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa tuhuma za kumuua John James (35), mfanyabiashara na mkazi wa Chanika.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, James amezikwa nyumbani kwao Kata ya Rung’abure wilayani Serengeti, mkoani Mara, wakidai chanzo cha kuuawa ni mzozo ulioibuka kati yao.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase in-aeleza tukio hilo lilitokea Februari 28, saa 2:05 asubuhi katika Kijiji cha Kikwete, Kata ya Marumbo wilayani Kisarawe, mkoani Pwani.

Polisi katika taarifa inasema askari wa idara ya misitu wakiwa doria walimjeruhi kwa kumpiga risasi kichwani mfanyabiashara huyo.

“Awali, kabla ya tukio la matumizi ya si-laha, John alikaidi amri ya kukamatwa na askari hao wa idara ya misitu na kuzuia pikipiki yake isichukuliwe, ndipo vurugu zilitokea wakati wa kumkamata mtuhumiwa huyo na kusababisha ma-tumizi ya silaha,” inasema taarifa ya poli-si.

Kamanda Morcase amesema matumizi ya silaha imekuwa sababu ya kumpiga risasi eneo la kichwani mtu huyo na ali-fariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali.

Taarifa inaeleza kuwa, askari hao wana-shikiliwa kwa tuhuma za mauaji na baada ya upelelezi kukamilika hatua zaidi za kisheria zitafuata.

Siyo tukio la kwanza

Matukio ya askari wa idara ya misitu kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji siyo la kwanza, Januari 2024, wanne wilayani Geita walishikiliwa na kwa tuhuma za kumuua mwananchi kwa kumpiga risasi alipokuwa akiokota kuni bila kibali katika msitu wa Samina uliopo wilayani humo.

Desemba 2, 2024 askari watatu wa idara hiyo na mgambo wanne walishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Grace Mussa (4), katika Kijiji cha Mpanda Mlowoka wilayani Kaliua.

Kauli ya ndugu, mashuhuda

Emanuel Charles, ambaye ni ndugu wa James akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu amesema alipigwa risasi akiwa hana mkaa aliodaiwa kusafirisha.

“Walitaka kumnyang’anya pikipiki yeye hakukubali kwa sababu hana kosa lolote, wamemuua. Tumeshamzika nyumbani Serengeti. Serikali ya Wilaya ya Kisarawe imetusaidia jeneza na usafiri wa kwenda kumzika, hatujui hatima ya ndugu yetu. Marehemu ana watoto watatu, Serikali imetuambia watasoma bila shida, mam-bo mengine hawakutuambia,” amesema.

Omary Mgunga, dereva wa bodaboda eneo la Kisarawe anadai walikuwa na James wakinywa chai huku pikipiki zao wakiwa wameziegesha jirani na wali-pokaa.

“Ghafla tuliona askari wa TFS na gari lao wanapita wakiwa wanne, baada ya mu-da wakarudi wanataka kuchukua pikipiki zilizokuwa kijiweni, wenzetu wengine walikimbia kunusuru pikipiki zao, James yeye hakukimbia askari wakawa wana-taka kuchukua pikipiki akagoma akisema hana kosa lolote,” amedai Mgunga.

Anadai kutokana na James kuzuia pik-ipiki kuchukuliwa, askari walifyatua risasi angani na baadaye risasi ilimpiga kwenye paji la uso kijana huyo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kikwete, wilayani Kisarawe, Selemani Giliwa amesema akiwa shambani alipigiwa simu na wananchi baada ya kusikia milio ya risasi.

Amesema taarifa hizo zilimfanya akim-bilie eneo la tukio ambako akikuta James amepelekwa hospitali akaelezwa askari wa mistu ndio wametekeleza jambo hilo.

“James hakuridhia pikipiki yake ikamat-we kwa sababu yeye hakuwa na mkaa na alikutwa kijiweni anasubiri abiria sasa askari wale walipotaka kumlazimisha atoe pikipiki walifyatua risasi hewani na baadaye kumfyatulia na kumjeruhi kichwani askari walikuwa wanne kama wananchi wangu walivyonieleza,” amesema.