London, England. Meneja wa Arsenal,Mikel Arteta amefichua kuwa amesikitishwa na klabu hiyo kutosajili mchezaji yeyote katika la usajili la majira ya kiangazi lililofungwa Januari 31, 2025.
Ilitegemewa Arsenal ingesajili mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji katika dirisha hilo dogo la usajili la Januari kufuatia majeraha ambayo yatamuweka Gabrie Jesus hadi mwisho wa msimu huku Bukayo Saka akiwa nje akiuguza maumivu ya misuli.

Arteta ambaye jana timu yake ilicheza mechi ya marudiano ya nusu fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Newcastle United, alisema kuwa sababu za kiuchumi zimechangia timu yake kutofanya usajili.
“Tulikuwa na nia ya wazi ambayo ni siku zote dirisha linapofunguliwa, kusaka fursa za kuimarisha kikosi chetu kwa wachezaji ambao wanaweza kutupa matokeo.
“Kwa wachezaji walio majeruhi, tumeathirika na hatujafanikiwa. Tumesikitishwa katika namna hiyo lakini pia tulikuwa makini sana kwamba tunahitaji kuleta aina fulani ya wachezaji na tulipaswa kuwa na nidhamu ya hilo pia. Nadhani ndivyo tulivyokuwa.
“Ni katika wasifu, mchezaji ambaye tunaamini anaweza kutuweka bora zaidi. Kiuchumi kuna njia nyingi, mambo mengi ambayo tunapaswa kukaa nayo kwenye mstari ambao umetufanya tuwe hapa na kuanzia hapo kujaribu kuimarika,” alisema Arteta.
Katika dirisha hilo dogo la usajili la Januari, wachezaji watatu waliondoka Arsenal ingawa wote walikuwa hawapo katika mipango ya Arteta kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Arsenal ilimpoteza beki wa kati Ayden Heaven (17) aliyetimkia Manchester United na mwingine ni Josh Robinson (20) aliyejiunga na Wigan Athletic.
Mchezaji mwingine ambaye Arsenal ilimfungulia milango katika dirisha dogo la usajili ni Marquinhos ambaye alijiunga na Cruzeiro ya Brazil.
Katika dirisha hilo dogo, Arsenal ilitajwa kuwania saini ya mshambuliaji wa Astin Villa, Ollie Watkins lakini dau ala Pauni 40 milioni ambalo ilitoa, lilikataliwa ambapo ilitajiwa dau la Pauni 60 milioni ililoligomea.
Baada ya kumkosa Watkins, inaripotiwa kwamba Arsenal ilijaribu kumsajili kwa mkopo nyota wa zamani wa Chelsea, Alvaro Morata kutoka AC Milan lakini mchezaji huyo akatimkia Galatasaray ya Uturuki.