Arsenal kicheko Saka akianza mazoezi ya kurejea

Winga wa Arsenal, Bukayo Saka ameonekana kuwa katika hatua nzuri ya kurejea uwanjani baada ya picha kumnasa akifanya mazoezi ya gym katika kambi yao huko Dubai.

Picha hizo zinaonyesha kovu lililobaki kwenye mguu wake baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye paja lake.

Kovu hilo linaonekana kwenye mguu wake wa kulia, juu ya goti.

Saka anatarajiwa kurejea uwanjani mapema mwezi Machi, mwaka huu baada ya kuumia nyama za paja mwezi Desemba, mwaka jana.

Kikosi cha Mikel Arteta kimeweka kambi katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu tangu wiki kikijiandaa na michezo ya Ligi Kuu England inayotarajiwa kurudi wikendi hii.

Winga huyo alipata jeraha hilo katika mchezo dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana ambapo alifanyiwa mabadiliko kipindi cha kwanza.

Endelea kufuatilia Mwananchi.