
Mahakama ya Juu ya Argentina siku ya Jumanne, Juni 10, imeidhinisha hukumu ya rais wa zamani Cristina Kirchner, kiongozi mashuhuri katika siasa za Argentina kwa miaka 20, kifungo cha miaka sita jela na kutostahiki maisha yake yote kwa udanganyifu wakati wa utawala wake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika hukumu yake, Mahakama imezingatia kuwa hukumu zilizotolewa katika kesi ya kwanza na ya pili “zilitokana na ushahidi wa kina uliotolewa.” Kwa hivyo, “imetupilia mbali rufaa” ya Cristina Kirchner, ambaye, kwa sababu ya umri wake (72), alipaswa kuepuka kufungwa na kupewa kifungo cha nyumbani.
Mahakama ya Juu ilipangwa kutoa uamuzi kuhusu rufaa iliyowasilishwa na Bi Kirchner dhidi ya hukumu yake mwishoni mwa mwaka 2022 hadi miaka sita gerezani na kutostahiki maisha yake yote kwa “udanganyifu dhidi ya utawala wa umma” wakati wa utawala wake. Hukumu hiyo ilikubaliwa katika kesi ya pili mnamo mwaka 2024.
“Haki. Mwisho,” ametoa maoni rais wa kiliberali Javier Milei kwenye ukurasa wake wa X muda mfupi baada ya hukumu.
“Jamhuri inafanya kazi, na wanahabari wote wafisadi, washirika wa wanasiasa waongo, wamefichuliwa katika uhalifu wao kuhusu kile kinachoitwa mkataba wa kutokujali,” ameongeza, akimaanisha uvumi kwamba sekta mbalimbali za ulingo wa kisiasa zilishirikiana ili kuepusha hukumu kwa Bi Kirchner.
Bi Kirchner, ambaye anakanusha makosa yoyote, mara kwa mara ameshutumu “mateso ya kisiasa na mahakama” wakati wa kesi hizi zinazolenga “kumtenga” na siasa. “Wanataka nifungwe au nife,” alitangaza tena kwenye mkutano wa Jumamosi, akimaanisha shambulio alilonusurika mnamo mwaka 2022.
Mamia kadhaa ya wafuasi wa Bi Kirchner, walikusanyika tangu asubuhi mbele ya makao makuu ya chama cha Justicialist, walionyesha uungaji mkono wao na hasira kwa tangazo la uamuzi huo, shirika la habari la AFP limebaini. Bi Kirchner alitarajiwa kuwahutubia wafuasi wake siku ya Jumanne alasiri.