Araghchi: Iran haitafanya mazungumzo na Marekani maadamu mashinikizo yapo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, katika mkutano wa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, mjini Tehran, amesea hakuna mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yatakayofanyika maadamu Washington inaendeleza sera  sera ‘Mashinikizo ya Juu Zaidi’ dhidi ya Iran.