
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran na Pakistan zinaamini kuna uhusiano wa karibu kati ya kundi kijikundi cha kigaidi cha Jaish al Dhulm na utawala wa Kizayuni na zinasisitiza juu ya kupigana na kukabiliana nalo.
Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Iran, IRNA, Seyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo katika mkutano na waandishi habari siku ya Jumatano, mwishoni mwa ziara yake nchini Pakistani.
Amesema kuna uhusiano wa karibu kati ya hatua za kichokozi za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kuanza tena chokochoko za makundi ya kigaidi hususan Jaysh al-Dhulm (ambalo linajiita Jaysh al Adl) na hiyo ni ishara ya uhusiano wa karibu wa kundi hilo na Israel. Amesema Tehran na Islamabad zina azma ya kuimarisha hatua dhidi ya kundi kundi hilo la kigaidi.
Araghchi pia ameashiria namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyochukiwa nchini Pakistan na kusema kuna haja ya kuchukuliwa hatua za kusimamisha mashambulizi na jinai za utawala wa Kizayuni.
Araghchi pia ameashiria azma ya pamoja ya Iran na Pakistan katika kukabiliana na hali ya ugaidi na akasema: “Katikaa safari ya Pakistan zilibadilishna mawazo kuhusu eneo, suala la Afghanistan na hali ya ugaidi na ulazima wa kuchukuliwa hatua ya pamoja dhidi ya uovu huu.”
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema nchi mbili zinaweza kushurukiana katika nyuga za kiuchumi, kisiasa na kijamii.