Apple yasafirisha mamilioni ya simu za iPhone kutoka India ili kukwepa ushuru wa Donald

Takriban tani 600 za simu za iPhone zimerejeshwa kutoka India kwenda Marekani ili kuepuka ushuru wa forodha uliowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump. Kampuni ya Apple, inayotengeneza simu zake nchini China na India, inahofia kutozwa ushuru kwa China ambayo itasababisha bei ya bidhaa yake kuu kupanda. China inazalisha takriban 80% ya simu za iphone duniani, lakini India inataka kushindana na inaona hii kama fursa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Bangalore, Côme Bastin

Takriban simu za iPhone milioni 1.5 zimesafirishwa kutoka India kwa ndege sita za mizigo katika wiki za hivi karibuni. Lengo: kusambaza bidhaa hiyo katika soko la Marekani kabla ya ushuru mpya wa forodha kuanza kutumika. Hatimaye, kuagiza kutoka India kwa ushuru wa 26%, ikilinganishwa na zaidi ya 50% kwa iPhone “zilizotengenezwa China“. Mamlaka ya viwanja vya ndege imepunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuwezesha shughuli hiyo.

Kulingana na UBS, simu ya iPhone iliyotengenezwa China inaweza kugharimu karibu euro 2,000 nchini Marekani ikiwa hatua za ulinzi za Donald Trump – ambazo zimesitishwa kwa siku 90 – zitatekelezwa kikamilifu. Viwanda vitatu vya iPhone nchini India, vilivyoko Chennai na Bangalore, vimekuwa vikifanya kazi kwa uwezo kamili tangu kuongezeka kwa vita vya kibiashara.

Serikali ya India, ambayo imekuwa ikitetea “make in India” kwa miaka kumi bila mafanikio yoyote ya kweli, inataka kunufaika na faida yake mpya ya ushindani dhidi ya Beijing. Tatizo moja kubwa linabaki: uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo. Leo, India inatengeneza 15% ya simu za iPhone, na Apple inatarajia kufikia 25% ifikapo mwaka 2027. Kwa hivyo China itasalia kuwa kiwanda kikuu cha Apple katika muda wa kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *