Ansarullah yapuuza hatua ya Marekani kuiweka harakati hiyo kwenye orodha yake ya magaidi

Ansarullah ya Yemen imepuuza uamuzi wa hivi karibuni wa Marekani wa kuiweka harakati hiyo ya Muqawama kwenye orodha ya makundi yake ya kigaidi na kusema kuwa, kujumuishwa kwenye orodha ya marafiki wa Marekani ni aibu na tishio kubwa zaidi kuliko hata ugaidi wenyewe.