Ansarullah waapa kuchukua hatua ya kijeshi iwapo mpango wa Trump dhidi ya watu wa Gaza utatekelezwa

Kiongozi wa harakati ya Ansarulllah nchini Yemen, Abdul-Malik al-Houthi, ameapa kuchukua hatua za kijeshi mara moja iwapo Marekani na Israel zitaanzisha mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza au kutekeleza mpango wa kuwahamisha kwa mabavu wakazi wa eneo hilo.