Ansarullah: Muhammad al Dhaif alisabilia maisha yake kwa ajili ya kuikomboa Palestina

Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa mkono wa pole kufuatia tangazo la kuuliwa shahidi Muhammad al Dhaif na kusema kamanda huyo Mpalestina alijitolea maisha yake kwa ajili ya kukomboa ardhi ya Palestina.