Angola yashtushwa na kikao kati ya Rais Kagame na Thisekedi Qatar

Nchi ya Angola, ambayo inaongoza katika upatanishi wa mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inasema ilishtushwa na kikao cha rais Felix Thisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, siku ya Jumanne nchini Qatar.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Angola Tété Antonio amesema, rais João Lourenço alishangazwa kuona viongozi wa DRC na Rwanda wakikutana chini ya uongozi wa nchi ya Qatar.

Aidha, ameongeza kuwa, Angola ambayo haikuwa na taarifa kuhusu kikao cha Tshisekedi na Kagame, inaendelea na mchakato wa upatanishi kwa mujibu wa mchakato wa Luanda, kuwezesha mazungumzo ya ana kwa ana kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23.

Rais wa Angola João Lourenço, ambaye nchi yake inaoongoza upatanishi wa mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa na rais Felix Thisekedi.
Rais wa Angola João Lourenço, ambaye nchi yake inaoongoza upatanishi wa mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa na rais Felix Thisekedi. © https://www.facebook.com/photo?fbid=869439951901366&set=pcb.869441515234543

Mazungumzo hayo, yalikuwa yamepangwa kuanza siku ya Jumanne, wiki hii, lakini waasi wa M 23 walijiondoa, baada ya waasi hao kulalamikia hatua ya umoja wa Ulaya, kuwawekea vikwazo viongozi wake.

Haya yanajiri wakati waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda wakipuuza wito wa usitishwaji vita na kuondelea kusonga mbele, ambayo siku ya Jumatano waliudhibiti mji wa kimkakati wa Walikale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *