
Karibia watu 108 wamefariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu nchini Angola tangu mwanzoni mwa mwaka huu kulingana na taarifa ya wizara ya afya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Takwimu hizi zimetolewa wakati huu idadi ya vifo ikiripotiwa kuongezeka katika siku za hivi punde.
Hadi kufikia sasa, visa 3,147 vya kipindupindu vimethibitishwa kwenye taifa hilo tangu tarehe saba ya mwezi Januari.
Kulingana na Wizara ya afya kwenye taifa hilo, karibia nusu ya visa vyote vya maabukizo ya kipindupindu vimeripotiwa katika Mji Mkuu Luanda. Mamlaka inasema walioambukizwa ni wa umri kati ya miaka miwili hadi 100.
Watu 48 wamethibitishwa kufariki mjini Luanda na wengine 43 katika eneo la Bengo, mpaka na mji mkuu.
Kipindupindu ni ugonjwa wa tumbo ambao husambaa kupitia kwa chakula na maji machafu na husababisha mgonjwa kuharisha, kutapika pamoja na maumivu ya viungo.
Mtu aliyeambukizwa anaweza kufariki haraka baada yake kuambukizwa iwapo hatopata matibabu ya haraka.