Amorim ampa masharti haya bosi Man United

Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim amemtaka mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Jason Wilcox kushirikiana naye vilivyo na kuwa makini katika dirisha lijalo la usajili ili kufanikisha mpango wa kuirudisha timu hiyo katika mstari.

Man United ambayo inaenda katika dirisha lijalo la usajili la majira ya kiangazi na uhitaji wa maboresho makubwa kwenye kikosi chao huku ikiwa kiasi kidogo kilichotengwa kama bajeti, italazimika kusuka upya timu kwa sababu ya hali yao msimu huu kuwa mbaya.

“Tunahitaji kuwa na muunganiko mzuri sana, nilipokuwa Sporting Lisbon, mazingira yalikuwa ni tofauti, hapa mambo ni tofauti kuanzia ushindani na ukubwa wa timu, hivyo tunahitaji kuwa makini sana katika kusajili. Tunahitaji kujua mfumo wetu, jinsi tunavyocheza, na wachezaji lazima wawe kamili kwa kuingia katika mifumo hiyo. Tunajua tunachofanya kwa sasa, acha tuone msimu ujao.”

Man United imekuwa ikihusishwa na wachezaji kadhaa akiwemo mshambuliaji wa Sporting, Victor Gyokeres, na kiungo wa Borussia Dortmund, Felix Nmecha, lakini usajili wowote kati wachezaji hawa hautakamilika hadi itakapouza kwanza.

Miongoni mwa wachezaji wanaodaiwa kuwaweka sokoni ni pamoja na Marcus Rashford, Antony na Jadon Sancho ambao wote kwa sasa wanacheza kwa mkopo katika timu nyingine (Sancho yuko Chelsea, wakati Rashford yuko Aston Villa).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *