Amani nchini Ukraine: Tofauti nyingi zajitokeza kati ya nchi za Ulaya na Marekani

Shirika la habari la Reuters limeweza kuoata nakala ya mapendekezo pingamizi kutoka maafisa wa nchi za Ulaya na Ukraine kuhusu makubaliano ya amani nchini Ukraine kama yalivyotakiwa na Marekani, kutoka suala la ardhi inayokaliwa hadi vikwazo vinavyolenga Urusi.

Imechapishwa:

Dakika 3

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo yaliyotokana na mazungumzo kati ya maafisa wa Marekani, Ulaya na Ukraine mjini Paris mnamo Aprili 17 na mjini London Aprili 23 yalifichua utendakazi wa diplomasia inayoendelea huku Rais wa Marekani Donald Trump akitafuta kumalizika kwa haraka vita nchini Ukraine. Ingawa baadhi ya tofauti zimeangaziwa na vyanzo vilivyo karibu na majadiliano, hati zilizoshauriwa na shirika la habari la Reuters zimeeleza tofauti hizo kikamilifu na kwa uwazi.

Hati ya kwanza ni pamoja na mapendekezo yaliyowasilishwa na mjumbe wa Donald Trump, Steve Witkoff, kwa wenzake wa Ulaya huko Paris, ambayo yalipitishwa kwa Ukraine, kulingana na vyanzo vilivyo karibu na majadiliano. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ameelezea mapendekezo hayo kama “mfumo mpana” wa kutambua tofauti za pande husika. Nakala ya pili iliandaliwa wiki moja baadaye wakati wa mazungumzo kati ya maafisa wa Ukraine na Ulaya huko London na kukabidhiwa kwa upande wa Marekani, vyanzo vimesema.

Maeneo yanayoshikiliwa, usalama, vikwazo…

Kuhusu suala la maeno yanayoshikiliwa nchini Ukraine, mapendekezo ya Steve Witkoff yanataka Marekani itambue udhibiti wa Urusi juu ya Crimea, peninsula ya Ukraine iliyotwaliwa na Moscow mwaka 2014, pamoja na kutambua kwa hakika udhibiti wa Urusi katika maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine ambayo inayadhibiti. Kinyume chake, hati ya Ulaya na Ukraine inaahirisha majadiliano yoyote ya kina juu ya eneo hilo hadi mwisho wa usitishaji mapigano, bila kutaja katika waraka huo utambuzi wa udhibiti wa Urusi juu ya eneo lolote la KiukreniUkraine.

Kuhusu usalama wa muda mrefu wa Ukraine, waraka wa Marekani unasema kwamba Ukraine itanufaika na “dhamana kali ya usalama,” huku mataifa ya Ulaya na mataifa mengine rafiki yakifanya kama wadhamini. Waraka huo haujasema zaidi na kubainisha kuwa Kyiv haitatafuta kujiunga na NATO. Hati nyingine ni mahususi zaidi, ikisema kwamba hakutakuwa na vikwazo kwa vikosi vya Ukraine na hakuna vizuizi kwa washirika wa Ukraine kuweka vikosi vyao vya kijeshi katika ardhi ya Ukraine – kifungu ambacho kinaweza kuiudhi Moscow. Pia inatoa dhamana dhabiti za usalama kwa Kyiv, ikijumuisha kutoka Marekani, na “makubaliano ya aina ya Ibara ya 5,” kifungu cha msingi cha ulinzi wa pande zote wa NATO.

Kuhusu hatua za kiuchumi, mapendekezo ya Steve Witkoff yanaeleza kuwa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi tangu kunyakuliwa kwa Crimea mwaka 2014 vitaondolewa kama sehemu ya makubaliano yanayojadiliwa hivi sasa. Mapendekezo ya kupinga, kwa upande mwingine, yanatazamia “kupunguza vikwazo hatua kwa hatua baada ya kuanzishwa kwa amani ya kudumu.” Vikwazo vinaweza kurejeshwa ikiwa Urusi itashindwa kuzingatia masharti ya makubaliano ya amani.

Hati iliyoandaliwa na nchi za Ulaya na Ukraine pia inapendekeza kwamba Ukraine inapaswa kupata fidia ya kifedha kwa uharibifu uliosababishwa wakati wa vita, kutoka kwa mali ya Urusi iliyohifadhiwa nje ya nchi. Nakala ya Steve Witkoff inasema tu kwamba Ukraine italipwa fidia ya kifedha, bila kutaja chanzo cha fedha.

Witkoff huko Moscow kwa mara ya nne

Marekani imekuwa ikifanya mazungumzo tofauti na Urusi na Ukraine kwa wiki kadhaa kwa lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano. Siku ya Ijumaa, Aprili 25, mjumbe wa Marekani Steve Witkoff alikutana na Vladimir Putin kwa mara ya nne tangu kuanza tena kwa uhusiano kati ya nchi zao mbili bila kutarajiwa katikati ya mwezi wa Februari kwa mpango wa Donald Trump. Majadiliano hayo ya saa tatu “yalisaidia kuleta pamoja misimamo ya Urusi na Marekani sio tu kwa Ukraine bali pia katika masuala mengine kadhaa ya kimataifa,” mshauri wa kidiplomasia wa rais wa Urusi amewaambia waandishi wa habari. Kulingana na yeye, “uwezekano wa kuanza tena mazungumzo ya moja kwa moja kati ya wawakilishi wa Urusi na Ukraine ulijadiliwa haswa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *