Na Mwandishi Wetu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo limemuachia Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe kwa dhamana baada ya kukamatwa kwa saa kadhaa usiku wa kuamkia leo kwa madai ya kutoa kauli chafu kwa viongozi wa Serikali.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, licha ya kuachiwa taratibu nyingine za kiuchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili zinaendelea na Kamwe atatakiwa kuripoti Aprili 21,2025.
Kamwe alishikiliwa na Polisi ikiwa ni siku mbili zimepite tangu adaiwe kurusha dongo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha katika hamasa kuelekea mchezo wao dhidi ya Tabora United uliopigwa jana.