Aliyeteuliwa na Trump kuwa balozi UN: Israel ina ‘haki kibiblia’ ya kuupora Ukingo wa Magharibi wa Palestina

Aliyeteuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani kuwa balozi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa amekuwa afisa wa karibuni zaidi wa serikali hiyo mpya kutangaza na kutetea imani kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel ina mamlaka na haki kwa mujibu wa maandiko ya Biblia ya kuunyakua Ukingo wa Magharibi wa ardhi ya Palestina unaoukalia kwa mabavu.