
Lungu alikuwa kiongozi wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika kati ya mwaka wa 2015 na 2021, wakati aliposhindwa kwa kishindo katika uchaguzina Rais wa sasa Hakainde Hichilema. Chama chake kimesema kwenye ujumbe kilichoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa rais huyo wa zamani, ambaye amekuwa akipokea matibabu maalumu nchini Afrika Kusini, alifariki dunia leo Alhamisi. Patriotic Front imesema binti ya Lungu na mwanasheria wa familia yake wamethibitisha kifo chake.
Aliingia madarakani mwaka wa 2015, baada ya kifo cha mtangulizi wake Michael Sata, na kujieleza kama “Mzambia wa kawaida aliyetoka katika maisha ya kawaida kabisa. Baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2021, Lungu alistaafu, na kisha akarejea katika siasa 2023, alipochaguliwa kuwa kiongozi na mgombea urais wa upande wa muungano wa upinzani ukiongozwa na chama cha Patriotic Front. Lakini Disemba mwaka jana, mahakama ya kikatiba ya Zambia ilitoa uamuzi kuwa hastahili kugombea muhula mwingine madarakani.