“Alidhihiri katika kipindi sahihi cha historia” shahid Nasrullah kwa mtazamo wa watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X

Parstoday: Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wametuma ujumbe mbalimbali kwenye mtandao huo kumsifu shahid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon.

Kuuawa shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kumeitikisa mitandao ya kijamii na kusababisha kushuhudiwa wimbi kubwa la maoni ya kila namna. Miongoni mwa mitandao hiyo ya kijamii ni ule wa X ambao zamani ulikuwa unajulikana kwa jina la Twitter. Hapa chini tunakuleteeni baadhi ya maoni hayo:

Sayyid Hassan Nasrullah alikuwa mlima imara

Tassadduq Hussain ametuma picha ya shahid Sayyid Hassan Nasrullah na kumtaja kuwa alikuwa ni mlima imara usiotetereka na kuandika:

Wametumia tani 83 za miripuko ili kukuua shahidi kwa sababu ulikuwa ni mlima usiotetereka.

Mpambanaji kwa ajili ya Ghaza

Mtumiaji mwingine anayejulikanakwa jina la Uncle Hoz naye emetuma picha kuhusu kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na kuandika:

Kila unavyoangalia, utaona kuwa Hassan Nasrullah emeuawa kwa sababu alisimama imara kuitetea Ghaza. Wakati ambapo hakuna kiongozi yeyote wa nchi ya Kiarabu aliyefanya hivyo.

Nasrullah: Shahidi wa kipindi sahihi cha historia

Kim Iversen, mtangazaji maarufu wa televisheni nchini Marekani ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kuhusu shahid Sayyid Hassan Nasrullah na kuandika:

Haijalishi unaiangalia vipi Hizbullah lakini ni muhimu tukumbuke kwamba lengo linalowafanya waishambulie Israel ni kuishinikiza iache kufanya mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina. Nasrullah ameuawa kwa kifo hasa cha shahidi aliyekuwa anawahami na kuwalinda watu wasio na ulinzi. Alikuwepo katika kipindi sahihi cha historia.

Amekuwa sababu ya umoja baina ya Waislamu

Hussin Makke, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kiislamu naye ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X na kuielezea hivi shakhsia ya shahid Nasrullah:

Kiongozi wa Kishia ameuawa katika kuwalinda na kuwatetea ndugu zake wa Kisuni.